Alhamisi, 28 Mei 2015

JE UNAFAHAMU UMUHIMU WA SAIKOLOJIA YA ELIMU? SOMA HAPA


Saikolojia ya elimu ni tawi la taaluma ya saikolojia linaloshughulikia masuala ya elimu, tawi hili linachunguza jinsi mwanafunzi anavyojifunza mambo mbalimbali ya kielimu, kijamii na kiutamaduni na namna bora ya kumfundisha. Sasa hebu tuangalie tawi hili lina umuhimu gani? Au kuna umuhimu gani wa mwalimu kujua saikolojia?

Umuhimu wa saikolojia ya Elimu
1).Hii humsaidia mwalimu kujua tabia za mwanafunzi na kujua ni kwa njia au mbinu gani anaweza kuzitumia ili tendo la kujifunza litokee na pia kujua sababu zinazoweza kufanya tendo la kujifunza lisiimarike mfano wanafunzi hutofautiana sana kutokana na malezi waliyolelewa au mahala walipotokea, hivyo kama mwalimu ukishajua tofauti hizi utajua utumie mbinu zipi ili kuhakikisha kuna usawa wa elimu au ulichokifundisha kimeeleweka kwa wote bila ya kubagua mwenye uwezo mkubwa au mdogo.
2) Husadia pia kujua jinsi ubongo au akili ya binadamu inavyotumika katika tendo la kujifunza. Kujua huku kutafufua njia na mbinu mbalimbali kuhakikisha kinachofundishwa kimefanikiwa.
3) Husaidia kumjua vema mwanafunzi wako na kujua jinsi gani utamsaidia ili ajifunze vema zaidi.
4) Itakusaidia kufahamu matatizo yanayokwamisha mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji na kujua jinsi gani utaweza kuyatatua.
5) Kwa kufahamu saikolojia na tabia za wanafunzi wako utaweza kuwaandaa vema na kuwapa motisha ili walipende somo na kuwachochea inapobidi. Mfano unaweza kutumia mifano mizuri ya kile wanafunzi wanachokipenda ili kuwafanya wawe na furaha na umakini na kile unachokifundisha.
6) Utajua kama mwanafunzi ameelewa au hajakuelewa hata kama amekaa kimya bila ya kukuuliza au kusema lolote. Kuna wanafunzi huwa na uoga wa kuuliza swali pale anaposhindwa kuelewa sehemu fulani, hivyo kama una ujuzi wa saikolojia hali hii unaweza kuigundua kwa wanafunzi wako na kuirekebisha.

Kwa upande wangu nina hayo machache, ikiwa una lolote la kuongezea jisikie huru kuacha maoni yako kwani tuko pamoja katika kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali.

UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA


Ndugu wana UDPSA na wengine Makala hii itatusaidia Kujifunza kuhusu Saikolojia. Wengi kati ya watu wanaosumbuliwa na matatizo yanaoitwa ya dunia ni wale wanaopambana na nguvu zao bila kujua. Kwa kutumia akili zao vibaya, hujitesa kwa kufikiri na kutafsiri vibaya matukio ya kila siku yanayotokea duniani.

Kwa mfano, tukizungumzia kufa ambapo watu wengi wanaamini kwamba ni jambo baya, kuna wengine wanaona ni zuri ndiyo maana wapo wanaojiua, na kama tukisema vita ni hatari, bado kuna watu wanafurahia vita kwa vile si wote wanaowahurumia wafao vitani hata kama wataona maiti zao barabarani kwa wingi.
Kama nilivyosema, duniani kuna nguvu mbili, ambazo ni za watu wenyewe na za ulimwengu, hii ina maana kuwa hata mawazo ya mwanadamu ni nguvu na mtu anaposumbukia kuwaza jambo fulani kwa undani kiasi cha kuumiza moyo wake anakuwa anashindana na nguvu zake mwenyewe.
Ifahamike kuwa kadiri mwanadamu anavyozidi kuongeza nguvu ya kufikiri, iwe kwa kukua kimwili, kusoma na kujifunza mambo mengi zaidi, kwa asili anakuwa anaongeza nguvu ambazo asipokuwa makini anaweza kufa akishindana nazo badala ya kuzitumia katika kumsaidia kimaisha.
Kwa mfano, watu kutoka kabila la Wabarabeigi wanaopatikana mkoani Manyara, nchini Tanzania wanaishi maisha ya kuwinda wanyama na kula mizizi ya porini, hawawezi kukaa wakifikiri jinsi ya kupata gari kwa kuwa kwao gari halina maana. Kwao maendeleo ni kuwinda na kuzaliana.
Kwa maana hiyo linapokuja suala la maisha magumu litatokana na ukame na wala si ukosefu wa mitaji au kazi. Hawa hawawazi magari kwa sababu hawajajifunza umuhimu wake, hawajui umuhimu wa kuwa na zahanati, hospitali na wala bei ya mafuta haiwasumbui. Lakini kwa Wachaga waliozoea umeme wakikosa huduma hiyo kwao hilo litakuwa ni tatizo kubwa litakalowakosesha usingizi.
Vivyo hivyo, kwa watu waliozoea kutibiwa kwa sindano na vidonge, wakikosa tiba hizo itakuwa rahisi kwao kufa, kwa sababu akili zao zinatafsiri ukosefu huo kama tatizo kubwa kwao, lakini haiwi hivyo kwa Wasukuma wanaoishi maporini kusikokuwa na hospitali za rufaa wala umeme.
Tafsiri ya hili ni nini? Ni fikra zitokanazo na kujua mambo na namna ya kuyawaza. Watu wengi siku hizi wanajua utajiri, wanafahamu nini maana ya afya, wanaelewa umuhimu wa maendeleo lakini siyo wote wenye uwezo wa kukutana na changamoto hizo na kupata matokeo sahihi ya kile wanachokifahamu.
Kwenda hospitali kupimwa na kuambiwa kuwa una Kansa, Ukimwi, Kisukari, Pumu, TB na magonjwa kama hayo, siyo jambo linalowasaidia wengi kwa vile hawajui hatua ya kuelekea kwenye ujuzi huo wa mambo. Hapa ndipo elimu ya saikolojia inapohitajika ili iweze kumsaidia mtu anayejua mambo hayo namna ya kuyakabili, kuyaendeleza na kupata mafanikio.
Jambo la kusikitisha ni kwamba watu wengi wanaofahamu mambo hawafaidiki nayo na pale wanapojaribu kutumia ujuzi wao walioupata shuleni, wanajikuta wanaingia kwenye mapambano ya nguvu ya vile wanavyovifahamu.
Watu wengi leo hawalali usiku kucha wakipambana na yale waliyoyafahamu, utakuta mtu kakonda kwa sababu katambua mpenzi wake si mwaminifu, anakesha akilia bila kujua afanye nini kumaliza tatizo.
Mtu mwingine anakonda kwa sababu ni maskini, hana mtaji na ajabu nyingine kuna wanaosumbukia hata kasoro za maumbile yao ambazo wameumbwa nazo!

Get to know The History Wilhelm Wundt


Wilhelm Maximilian Wundt (16 August 1832 – 31 August 1920) Wundt was born at Neckarau,he was a German physician, physiologist, philosopher, and professor, known today as one of the founding figures of modern psychology. Wundt, who noted psychology as a science apart from biology and philosophy, was the first person to ever call himself a psychologist.He is widely regarded as the "father of experimental psychology". In 1879, Wundt founded the first formal laboratory for psychological research at the University of Leipzig. This marked psychology as an independent field of study.

By creating this laboratory he was able to explore the nature of religious beliefs, identify mental disorders and abnormal behavior, and find damaged parts of the brain. In doing so, he was able to establish psychology as a separate science from other topics. He also formed the first academic journal for psychological research, Philosophische Studien, in the year 1883.

PICHA ZA ZIARA YA BACK 2 LIFE SOBER KIGAMBONI

Karibu katika makala hii Iliyoandikwa na Mhariri FUNDU,AHMED Y. Hii ni ziara iliyofanywa huko na Wanafunzi wa Psychology kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam, Walipotembelea moja ya Sober za watu walioathirika na madawa ya kulevya kama Cocain,Heroin,Marijuana na madawa mengineyo ya kulevya. Msafara uliongozwa na Kiongozi mstaau wa Association ya UDPSA Bw.Charles Wisize pamoja na Mwnyekiti wa sasa wa UDPSA Bw.Mshana Goefrey. Kama wanasaikolojia kutoka katika chuo kikuu cha Dar es salaam tulijifunza mengi tulipotembelea kituo hicho cha watu walioathirika na madawa ya kulevya, moja ya mafunzo hayo ni kujua athari Hasi za madawa ya kulevya kiafya na kwa maendeleo ya jamii kwa ujumla. Sisi kama taifa la kesho la vijana  inatupasa kujua kuwa matumizi ya madawa ya kulevya ni adui mkubwa wa maendeleo. Tujaribu kuiasa jamii na vijana wenzetu kuhusu athari za madawa ya kulevya.


 Picha ya pamoja iliyojumuisha wanafunzi kutoka katika chuo kikuu cha Dar es salaam na waathirik wa madawa ya kulevya kutoka katika kituo hicho kinachoitwa Back 2 life sober house.




kuanzia kulia ni Mhariri wa makala hii Bw.Fundu,Ahmed Y. wa pili ni ndugu Lema, watatu ni Hakika Rashid na wanne ni Karia Peter wote kutoka katika chuo kikuu cha dar es salaam



 baada ya msafara ilitupasa kuwaaga na kuondoka katika makazi yetu







Jumatano, 27 Mei 2015

B. F. Skinner Biography (1904-1990)


B. F. Skinner was an American psychologist best-known for his influence on behaviorism. Skinner referred to his own philosophy as 'radical behaviorism' and suggested that the concept of free will was simply an illusion.

All human action, he instead believed, was the direct result of conditioning.

In this operant conditioning process, actions that are followed by good consequences are reinforced and therefore those behaviors are more likely to occur again in the future. Behaviors that result in negative consequences, on the other hand, become less likely to occur again.

Among his many discoveries, inventions, and accomplishments were the creation of the operant conditioning chamber (aka the Skinner Box), his research on schedules of reinforcement, the introduction of response rates as a dependent variable in research, and the creation of the cumulative recorder to track these response rates.

In one survey, Skinner was named the most influential psychologist of the twentieth-century.
Birth and Death:

Born: March 20, 1904

Died: August 18, 1990
Biography:

Burrhus Frederic Skinner was born and raised in the small town of Susquehanna, Pennsylvania. His father was a lawyer and his mother a homemaker and he grew up with a brother who was two years his junior.

He later described his Pennsylvania childhood as "warm and stable." As a boy, he enjoyed building and inventing things; a skill he would later use in his own psychological experiments. His younger brother Edward died at the age of 16 due to a cerebral hemorrhage.

During high school, Skinner started to develop an interest in scientific reasoning from his extensive study of the works of Francis Bacon. He went on to receive a B.A. in English literature in 1926 from Hamilton College. After earning his undergraduate degree he decided to become a writer, a period of his life that he would later refer to as the "dark year." During this time he wrote only a few short newspaper articles and quickly grew disillusioned with his literary talents, despite receiving some encouragement and mentorship from the famed poet Robert Frost.

While working as a clerk at a bookstore, Skinner happened upon the works of Pavlov and Watson, which became a turning point in his life and career. Inspired by these works, Skinner decided to abandon his career as a novelist and entered the psychology graduate program at Harvard University.